18th May 2012    [Contacts][Location]
Current Section: Events
 
 
 
  Government Website  

Past Events

KUTEULIWA KWA WAJUMBE WA BARAZA LA USHAURI WA USTAWI WA WANYAMA
Posted: 6th Nov 10

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Dk John Pombe Magufuli hivi karibuni aliteua Wajumbe wa Baraza la Ushauri wa Ustawi wa Wanyama linaloundwa chini ya kifungu Na. 5 cha Sheria ya Ustawi wa Wanyama sura Namba 154 ya mwaka 2008.

Katika uteuzi huo Waziri alimteua Profesa Donald Mpanduji Profesa wa Tiba ya Wanyama toka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Kitivo cha Tiba ya Mifugo Morogoro kuwa Mwenyekiti wa Baraza.  Aidha, Waziri aliwateua Wajumbe wengine tisa  kutoka taasisi/ Nyanja mbalimbali za   weledi ambao ni:

 (i)    Dr Lwitiko Mwakalukwa Dakatari wa Mifugo akiwa mwakilishi wa madaktari  wa Mifugo walioko sekta binafsi.

(ii)  Professor Jonathan Kabigumila mweledi wa Zoologia toka  Chuo Kikuu cha Dar es salaam

(iii) Bwana Alex Paul Magesa Mwanasheria wa Serikali toka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

(iv) Bibi Beatrice Masanilo mwanaharakati wa maadili ya Ustawi wa Wanyama toka Kikundi cha Wafugaji Chato.

(v)  Professor Abiliza Kimambo toka Idara ya Sayansi ya Wanyama ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Morogoro.

(vi)Dr. Victor Kakengi – Mtaalamu wa mienendo na tabia za Wanyama toka Taasisi ya Utafiti wa Wanyama Pori Tanzania (TAWIRI).

(vii)   Bi Johari Gessani Mwanaharakati wa kutetea haki za Wanyama toka Shirika lisilo la Kiserikali la kutetea haki za Wanyama (TSPCA)

(viii)    Dr. Thomas Kahema kutoka Chama cha kutetea Ustawi wa Wanyama (TAWESO)

(ix)Dr. Egyne Emmanuel – SP mteule wa Inspecta Jenerali wa Polisi toka Jeshi la Polisi Tanzania kikosi cha mbwa na Farasi.

 Kwa mujibu wa Sheria ya Ustawi wa Wanyama Katibu wa Baraza ni Mkurugenzi wa Wizara anayeshughulikia Ustawi wa Wanyama ambaye  ni Dr. Mohammed M. Bahari Mkurugenzi wa Idara ya Utambuzi na Usajili wa Mifugo Idara ambayo pia inasimamia ustawi wa wanyama.

 Idadi ya  Wajumbe wa Baraza kwa mujibu wa Sheria tajwa ni kumi na moja (11). Uteuzi wa Wajumbe utakuwa ni kwa kipindi cha miaka mitatu kuanza tarehe 9 Septemba 2010 na utaishia tarehe 8 Septemba 2013 ingawa wanaweza kuteuliwa tena.

 Kwa mujibu wa kifungu Namba ya 6 cha Sheria ya Ustawi wa Wanyama jukumu kubwa la Baraza ni kumshauri Waziri katika mambo yafuatayo:

(i)                Mambo yote ambayo kwa mujibu wa sheria sharti yaelekezwe kwenye Baraza.

(ii)              Masuala yote ambayo kwa minajili ya kusimamia sheria yanahitaji kumshauri Waziri.

(iii)            Mambo yote kwa ujumla yanayohusu Ustawi wa Wanyama

Katika kutimiza majukumu yake Baraza litakutana si chini ya mara nne kwa mwaka.

Baraza hili lilizinduliwa na Mheshimiwa Waziri tarehe 3 Novemba 2010 katika Hoteli ya Protea Courtyard Dae es Salaam.

hava durumu Rüya Tabirleri Okey Oyna hava durumu Günlük hava durumu Batak Oyna 101 Oyna Kombi Servisi indir Çizgi Film Şarkı Sözü Okey Oyna Altın Fiyatları Burçlar
TAWLAE
Posted: 4th Oct 06

Tanzania Association of Women Leaders in Agriculture and Environment (TAWLAE) held its Ten Years Anniversary, Conference and Annual General Meeting on 21st – 23rd AUGUST 2006 at Karimjee Conference Hall in Dar es Salaam.

 

 

 

 

 

 

 

hava durumu Rüya Tabirleri Okey Oyna hava durumu Günlük hava durumu Batak Oyna 101 Oyna Kombi Servisi indir Çizgi Film Şarkı Sözü Okey Oyna Altın Fiyatları Burçlar
   

 
                     more...
 
[Homepage] [Top] [Feedback]   Last Update:
18th May 2012